
L152 – Karibu Na Wewe, Mungu Wangu
“Nearer My God To Thee”
1
Karibu na wewe, Mungu wangu; Karibu zaidi, Bwana Wangu.
Siku zote niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
2
Mimi nasafiri duniani, Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
3
Yote unipayo yanivuta; Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe karibu na wewe; Karibu zaidi, Mungu wangu.
4
Na kwa nguvu zangu nikusifu, Mwamba, uwe maji ya wokovu;
Mashakani niwe, karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
5
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu; Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.
152
0 comments on “Karibu Na Wewe, Mungu Wangu”